30 minutes ago
MAAJABU YA SABUNI YA MAJIVU YA PUMBA NGUMU ZA MPUNGA
Karibu mpenzi msomaji wa makala hii, leo nimekuletea somo litakalokufunza jinsi ya kutengeneza sabuni ya unga ya kuoshea vyombo itokanayo na majivu ya pumba ngumu za mpunga. JINSI YA KUTENGENEZA 1-Chukua ndoo ya Lita ishirini (20 lts) Kisha uijaze pumba ngumu za mpunga,🪣2-mimina pumba chini Kisha zichome moto hadi ziwe majivu meupe pe, baada ya hapo yasage sage hayo majivu mpaka yawe unga mlaini, ❤️ Hatua ya 3- andaa chombo kikavu yachekeche ili kuondoa pumba ngumu,au uchafu mwingine,🪣 Hatua ya 4-chukua Omo (sabuni ya unga) kilo 2 weka ndani ya majivu huku ukikoroga taratibu hadi ichanganyikane vizuri, koroga Kwa kutumia mwiko mbao au kijiko kikubwa cha chuma,huku ukiwa umevaa barakoa Kwa usalama zaidi, 🟣 Hatua ya 5-Ongeza chapa maandashi vijiko 2 vya chakula, endelea kukoroga hadi vichanganyikane vizuri, 🟣Hatua ya 6 - Weka matone matano ya pafyumu au mafuta ya mimea kama vile Lemon oils, huku ukikoroga hadi harufu ienee vizuri kwenye unga wako, baada ya hapo funika Kwa muda wa dakika 10-15. Mpaka hapo sabuni yako ya kuoshea vyombo itakuwa imekamilika, tayari Kwa kufungashwa kwenye vifungashio kwenda sokoni. Asante kwa kuwa mwanafamila wetu, mimi ni wako Mwal. Andrew Mago, endelea kuwa nasi.
Read article